Tuesday, August 17, 2010

RAY C ATEMWA -K-LYNN KUPATA DEAL


Ray C

K-lynn
Inasemekana Ray C baada ya kuzinguana na Promota Sadat Muhindi, amejikosesha kiasi cha dola elfu32 za kimarekani, nikukumbushe kidogo
Mwanadada Ray C alisign deal na kampuni inayomilikiwa na Sadat Muhindi na katika mkataba huo alitakiwa kuwa balozi wa Kinywaji cha kuongeza nguvu/Energy Drink kinaitwa Dash, lakini kitumbua kilikuja kuingia mchanga baada ya mtafaruku kutokea baina ya Ray C na Saadat, na mpaka sasa hivi hakuna mwenye uhakika wa nani hasa alikua chanzo cha mtafaruku huo Coz kila upande unasema lake, Ray C anasema chanzo promota huyo alimtaka kimapenzi na yeye Ray C alichomoa, naye Saadat akapinga tuhuma za kumtaka Ray C kingono na zaidi hivi karibuni kwa mujibu wa chombo kimoja cha habari cha nchini kenya kinadai kuwa Promota huyo amdai kuwa Ray C ni teja wa madawa ya kulevya/junkie.
Back to the point ya Mwanadada mwenye kiuno bila mfupa kukosa dola elfu 32 usd,
kwa mujibu cheque iliyoshuhudiwa na chanzo chetu cha habari, Cheque imeandikwa tarehe 6 August na Adonai Enterprises Ltd, mkwanja ulioandikwa $32,000, Drawn to Rehema Yusuf(Ray C)
Promota huyo anasema, hiyo ni deal ya kwanza tu Ray C, na alipanga kumpatia Cheque hiyo, Jumatatu ya wiki iliyopita, (yaani siku mbili kabla hakijanuka kati yao) jamaa anaendelea kusema mkwanja ule ulikua kwa ajili ya Ray C kuji inua kimaisha kama balozi wa kinywaji chake cha Dash.
Saadat ambae ni mwanasiasa wa anaetokea pande za Kitale nchini Kenya, amesema kuwa moja wapo ya vitu walivyokubaliana na Ray C kuwa atakwenda kuchek afya yake Rehab.
(Rehab- ni sehemu ambayo anakwenda mtu aliyezidiwa na matumizi ya kupitiliza ya aina yoyote ya ulevi, na mtu huyo huwa anakwenda hapo ili kusaidiwa ushauri na matibabu ya kuacha ulevi huo)
Wakati huo huo:
Uongozi wa Kampuni inayomiliki Kinywaji cha Dash, umesema kuwa upo katika mazungumzo na mwanadada mwengine kutoka nchini Tanzania K-Lynn, na wakifikia makubaliano K-Lynn atatua nchini Kenya, kwa mujibu wa Kampuni hiyo K-Lynn yuo South Africa, Adonai enterprises wanampango wa kushoot Tangazo la Kinywaji chao kingine na Msanii kutoka Bongo anayejulikana na kama J.I na rapper wa Kenya Kenrazy na litafanyika kabla ya september.
Share/Save/Bookmark

No comments:

Post a Comment

 

.