Monday, October 4, 2010

AY AND MISS TRINITI



Wiki iliyopita AY pamoja na msanii kutoka Trinidad and Tobago Ms Trinity waielekea nchini Uganda na kushoot video yao mpya.

Wimbo huo ulirekodiwa katika studio za B.Hits jijini Dar es Salaam na video kufanyiwa ndani ya jiji la Kampala chini ya director Donald kutoka Dedac Production.

AY alinukuliwa akisema "Video itakuwa tayari ndani ya wiki mbili na watu wangu kokote waliko duniani wategemee good music kutoka kwangu na Ms Trinity.

Pia nilitumiwa muda huo nikiwa Kampala kwa kurecord video nyingine pamoja na mkali kutoka Uganda ajulikanae kwa jina la Ragga Dee.Video hiyo imefanywa na kampuni iitwayo JahLive ya nchini humo"alimalizia.

Ay pia anatarajia kurecord nyimbo zingine na wasanii wakubwa kama Sean Kingston mjamaika aliweka makazi yake nchini Marekani pamoja JMartins wa Nigeria hivi karibuni.

For more info:
http://www.ay.co.tz/
Share/Save/Bookmark

No comments:

Post a Comment

 

.