Thursday, March 31, 2011

MCHUMBA WA H-BABA FLORA MVUNGI ANASWA NA MWANAUME




Licha ya kuvishwa pete ya uchumba na nyota wa muziki wa Bongo bolingo fleva, Hamis Ramadhani Baba H. Baba, ‘diva’ wa tasnia ya filamu Bongo, Flora Mvungi amenaswa akichukuliwa maelezo (kutongozwa) na mwanaume mmoja wa Kizanzibar,Amani Jipya lina Full data.

Tukio la nyota huyo aliyefanya kweli kwenye muvi ya ‘True Love Never Die’kufumwa akitongozwa lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kamera ya Amani Jipya kummulika akiwa ‘klozi’ na jamaa huyo, Flora alisema kwa mara ya kwanza alikutana na ‘tozi’ huyo alipokuwa kikazi visiwani Zanzibar na tangu hapo jamaa amemganda kama ruba akimtaka kimapenzi.

“Aliniambia kuwa ni shabiki wangu mkubwa tulizungumza kidogo nikampa namba, tangu hapo amekuwa akinisumbua kwa kunitaka kimapenzi yaani hivi unavyomuona amesafiri kutoka huko kwao kuja kunifuata huku,” alisema Frola.

Flora alisema kwamba alishamwambia jamaa kama yeye amechumbiwa lakini haelewi wala hasikii na sasa anajuta kwa nini alitoa namba yake kwa jamaa huyo aliyemtaja kwa jina la Feisal.

Aidha, msanii huyo ambaye hivi karibuni aliripotiwa kubadili dini na kuwa Muislamu alisema kwamba jamaa anampigia simu kila kukicha na kutuma meseji za kumtaka kimapenzi.

“Nimechoka na hali hii wakati mwingine huwa nafikiria kubadili namba kwani nahisi siku ‘my love’ (H.Baba) akigundua patakuwa hapatoshi,” aliongeza.
HABARI KUTOKA GLOBAL PUBLISHER

Share/Save/Bookmark

No comments:

Post a Comment

 

.