Saturday, January 2, 2010

Bongo Fleva yatawala 2009

Katika kutathimini ,matokea ya muziki nchini watafiti wamesema 2009 bongofleva ilizidi kutawala na kushika chati kila kona ukilinganisha na miziki mengine kama dansi huku taarab na muziki wa injili ukiukimbiza .

Wasanii wa muziki huo walikuwa wakifumuka kila kukicha huku ushindani ukizidi kuwa mkubwa kila mmoja akitafuta staili yake ya kuteka soko.

Mwaka 2009 ulishuhudia wasanii wengi wakipata mialiko ya kufanya shoo kubwa nje ya nchi kwa wingi zaidi kuliko kipindi kilichopita pamoja na kuteuliwa kuwania tuzo tofauti nje ya nchi.

Ally Kiba ndiye msanii ambaye amekuwa na mafanikio zaidi mwaka huu kwani alifanya shoo nyingi zaidi Afrika na Barani Ulaya akifuatiwa na AY.

Huku mwanadada Jay dee akiendelea kuwaburuza kina dada,hii ni kutokana na umiliki wa bendi yake ya machozi bando ambayo inamuonesha yuli live zaidi, sambamba na kuachia vibao vyake redioni na runingani

Mbali na msanii huyo wengine waliofanya vizuri 2009 ni Chid Benz, AY, Ray C, Q-Chilla, Chege, Temba, Mrisho Mpoto,Mwanafalsafa Profesa Jay, Afande Sele,Fid Q, Matonya na Banana Zorro.Mwasiti, Maunda ,shaa, Witness
Share/Save/Bookmark

No comments:

Post a Comment

 

.