
Traki ya Njia Panda ambayo ni mali ya Barnabas ndiyo iliyomtambulisha, baada ya hapo akagonga kimya lakini sasa ameona its about time! Doreen Aurelian Ponera ‘Pipi’ anakunjuka kitaani akiwa kamili.
Pipi, ametambulisha wimbo wake wa kwanza unaokwenda kwa jina la Fisrt Time na ndani yake, hajampa mtu yeyote shavu. Amejaza vocal mwanzo mwisho!
Track hii ilianza kutambulishwa na kugongwa kwa mara ya kwanza Ijumaa ya wiki iliyopita na vituo kadhaa vya radio.
Pipi ni tunda kutoka Tanzania House of Talent (THT).
Hii hapa ndio track ya kwanza kumtambulisha Pipi kwenye ulimwengu wa muziki.
SIKILIZA HUO WIMBO HAPO JUU KULIA

No comments:
Post a Comment