Monday, August 9, 2010

MASTER KEY ANASEMAJE KUHUSU UWEZO WA WASANII WETU KUTUNGA MASHAIRI?

Wadau wenzangu mnaofuatilia kwa ukaribu game la mziki wa bongo, nimependa kushare na nyie wazo hili. nijuavyo mimi, mziki ulianza zamani sana kabla wengi wetu hatujazalia, na ukweli ni kwamba hata suala zima la kuimba nyimbo zinazohusu mapenzi lilianza zamani pia. kinachotokea hivi sasa ni kwamba kila msanii anatengeneza tenzi zake akigusia mambo ya kimapenzi zaidi na karibu kila mtu anaimba jambo lilelile.
mtazamo wangu ni kwamba naona kama mziki unakosa ladha ya ubunifu wa tenzi mpya. kila wakati watu huzungumzia visa kama kuachwa na mpenzi, kumlilia mpenzi warudiane, kumkanya mpenzi, n.k
yawezekana pia mapenzi yanatawala sehemu kubwa ya maisha lakini tuwe wabunifu wa kutengeneza mashairi yatakayoleta ladha tofauti katika mziki wetu wa bongo flava.
wadau naomba niwafahamishe pia wasanii wetu kwamba lazima wakubali kwamba unapokuwa na kipaji cha kuimba si lazima uwe unajua kutunga mashairi, kama kuna watu wenye uwezo wa kuandika mashairi mazuri basi wasanii wetu wakubali kwamba nayo hiyo ni fani ya watu.
tukifanya hivyo nina uhakika itasaidia, kwani kuwa msanii wa mziki si lazima uwe unajua kuandika mashairi.
tuzingatie, ni hayo tu katika kuchangia game la mziki wetu.
By Ray Ufunguo a.k.a Master Key
masterkey10@rocketmail.com
+255 713 059 037
Share/Save/Bookmark

No comments:

Post a Comment

 

.