Thursday, March 31, 2011

20 AFANYIWA PARTY YA NGUVU NA AFANDE SELE MOROGORO

Mfalme wa Rhymes 2004, Suleiman Msindi ‘Afande Sele’ amemwangushia bonge la pati, mshindi wa tuzo tano za Kili Music 2010/11, Abbas Hamis Kinzasa ‘20%’ au ‘Kombinenga’ (pichani) kwa lengo la kuupongeza ushindi wake, Amani Jipya linakuwa la kwanza kuwajuza.

Sherehe hiyo ya nguvu ilitwaa fursa Jumatatu ya Machi 28, mwaka huu nyumbani kwa Afande Sele, Misufini mjini Morogoro na kuhudhuriwa na waalikwa kibao.

Baadhi ya matukio ya ziada katika pati hiyo ni kitendo cha 20% mwenyewe kushika mapande ya ‘manyama’ kwa staili aliyoiita ya ‘kikombinenga’ na kutembea navyo hadharani huku akiongea na watu mbalimbali bila kujali ustaa wake.

Aidha, Afande Sele aliyemtaka msanii huyo ashuke Moro akitokea Tabora ili amfanyie sherehe, naye aliweka kando ufalme wake na kuunga mkono tabia ya ‘mwanaye’ huyo kwa kukamata kipande cha nyama kilichoonesha ni kuku huku akibadilishana mawazo na waalikwa.

Muziki wa ‘laivu’ ulipigwa kutoka kwa bendi isiyo na jina kubwa huku waalikwa waliokuwa wameketi kwenye viti vya plastiki wakijiachia kwa nyakati tofauti.

NI SALAMU ZANGU KWA JK
Akizungumzia ushindi wake wa tuzo tano za Kili katika mahojiano maalum na Amani, 20% alisema kuwa, ni salamu zake kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’.

“Hizi tuzo tano ni salamu zangu kwa Rais Kikwete kwamba kuna haja ya mimi na yeye kukutana kwa kuwa, wananchi wake waliomchagua mwaka jana wamenikubali kama walivyomkubali yeye, hivyo sote tumekubalika,” alisema 20%.

Alipoulizwa ni kwa nini hakuwepo Ukumbi wa Diamond Jubilee siku ya utaoji wa tuzo Machi 26, mwaka huu na badala yake akamtuma prodyuza wake Man Walter, msanii huyo alijibu:

“Mimi ni mtu wa watu, nafanya kazi ya muziki kwa lengo la kuwaburudisha na kuwaelimisha watu, sifanyi kwa sababu ya tuzo, hivyo naweze kusema kwamba waandaji hawakuwa makini kwa namna fulani.

“Wasanii tuna kazi za watu za miezi mitatu hadi minne mbele, sasa jamaa (waandaaji wa Kili) walinipa taarifa wakati tayari nilishachukua kazi za watu Tabora.

“Ni rahisi kutuma mwakilishi kwenye tuzo ndiyo maana alikwenda prodyuza wangu, lakini ni vigumu kumtuma mtu kwenye kazi za watu (shoo),” alisema 20%.

Aidha, msanii huyo aliongeza kwamba, akiwa Tabora alikuwa akifuatilia tuzo hizo kupitia runinga.

“Shoo ile nilikuwa naicheki na masela wangu kwenye runinga, nilishuhudia mpaka nilipopata tuzo ya nne hapo muda wa kazi ulifika nikapanda jukwaani, lakini masela walinijuza kwamba nimetimiza nguzo tano za Kiislamu,” alisema msanii huyo.

BABA YAKE AKEREKA, AMFOKEA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, msanii huyo aliweka hadharani kuwa, kutokuwepo Diamond Jubilee usiku ule kulimkera baba yake mzazi, Mzee Hamis Kinzasa ambapo alimpigia simu na kumfokea.

“Baba naye alikerwa sana na kitendo cha mimi kutokuwepo ukumbini. Alinipigia simu na kuniambia we ni mshen… sana, wenzako wamekodi magari kutoka Mkuranga kwenda Dar kukupongeza wewe haupo.”

Hata hivyo, 20% alisema kuwa, alimwelekeza baba yake huyo hali ilivyo ambapo alimwelewa, akapunguza mzuka.

ATOA TAMKO
Aidha, alisema alitaraji kutua Dar juzi Jumanne na kuzitwaa tuzo hizo hadi kwao Mkuranga na baadaye kuzirudisha jijini kwa programu nyingine, kisha akatoa tamko:

“Nachukua nafasi hii kuwaomba msamaha wazazi na mashabiki wangu, wanisamehe kwa kutoniona ukumbini.”

Katika tuzo hizo, 20% alivunja rekodi kwa kutwaa Msanii Bora wa Kiume, Muimbaji Bora wa Kiume na Wimbo Bora wa Afro-Pop.

Kwa upande wa nyimbo zake mbili za Ya Nini Malumbano na Tamaa Mbaya, zilishinda na kupokea tuzo kila moja.

MKANGANYIKO
Kwa mujibu wa Man Walter, 20% alishindwa kuhudhuria utoaji wa tuzo hizo kwa maelezo kwamba alikuwa ‘akishuti’ filamu huko Morogoro.

Maelezo hayo yanakinzana na haya ya 20% kuwa alikuwa kwenye shoo Tabora hivyo kusababisha watu kuhoji ukweli ni upi?
Share/Save/Bookmark

8 comments:

  1. I just like the valuable information you provide
    to your articles. I'll bookmark your blog and take a look at once more here frequently. I'm fairly
    sure I will be informed a lot of new stuff proper here!

    Good luck for the next!

    Here is my page Xtrasize Male Enhancement

    ReplyDelete
  2. When some one searches for his necessary thing, thus he/she wishes to be available that in detail, therefore that thing is maintained
    over here.

    Look into my webpage - Buy Slim Berry Max

    ReplyDelete
  3. Link exchange is nothing else however it is simply placing
    the other person's blog link on your page at appropriate place and other person will also do same in support of you.

    My weblog; Profit web system

    ReplyDelete
  4. Hello my loved one! I want to say that this article is
    amazing, great written and include almost all vital infos.
    I'd like to see more posts like this .

    Here is my web page Enduros Male Enhancement

    ReplyDelete
  5. Wow that was unusual. I just wrote an really long comment
    but after I clicked submit my comment didn't show up. Grrrr... well I'm not writing all that over
    again. Anyway, just wanted to say fantastic blog!

    Review my homepage :: Bellagenix review

    ReplyDelete
  6. Magnificent beat ! I would like to apprentice while you amend your site,
    how can i subscribe for a blog website? The account helped me a appropriate deal.
    I have been tiny bit familiar of this your broadcast provided brilliant
    transparent idea

    Here is my page :: Code Psn Gratuit (Www.dailymotion.com)

    ReplyDelete
  7. Why people still make use of to read news papers when in this technological globe all is available on net?


    Here is my page: Psn Code Generator

    ReplyDelete
  8. Wonderful post but I was wanting to know if you could write a litte more on this topic?

    I'd be very grateful if you could elaborate a little bit more. Cheers!

    Feel free to visit my homepage ... Codes Psn Gratuit (http://www.youtube.Com/watch?v=ojgPnR2Y9sk)

    ReplyDelete

 

.