Thursday, January 28, 2010

NEWS: G-SOLO MMILIKI WA STUDIO YA KAMA KAWA AANDIKA BARUA KWA RAISI



Yupo kitambo kwenye game,mshkaji anajulikana kwa jina la G-Solo.Mwaka huu amedai ni mwaka mzuri sana kwake kwakuwa amerudi tena na ana hasira sana kwani ataka kudhihirisha kama HipHop ni ya ukweli kabisa na inalipa kulinganisha na unavyoiwakilisha.

G-solo ameandika kitabu kuhusu bongo flava na ndani ya kitabu hicho kuna barua kwa rahisi kuhusu vilio vya wasanii wa bongo ..kaa tayari kwa kitabu hicho

GSolo amepingana na kauli ya wengi ya kwamba alipotea miaka hii ya karibuni na kudai alikuwa resi na masuala ya studio anayoimiliki pamoja na masuala mengine ya kifamilia.

"Nilikuwa na kazi sana achana na muziki,nina miliki studio ya Kama Kawa na ndio ilikuwa inachukua muda wangu mwingi,naamini sasa nimerudi na kwakweli lazima nidhihirishe ukweli kuhusu Hiphop"GSolo.

Alizidi kuchana na kusema anatarajia kuishangaza Tanzania na hata Dunia nzima kwakuwa sasa anatumia muda wake mwingi kwenye muziki na kumuachia mikoba yote prodyuza Q anayeisimamia studio yake kwa sasa.

"Nimepata prodyuza ambaye naamini ni prodyuza wa ukweli,sasa najiandaa kutoa wimbo wangu ambao ni maalumu kwa mtoto wangu na vilevile albam itafuta kwani kuna pini nyingi nimesharekodi chini ya lebo yangu ya Kamakawa.

Rapa huyu alikuwa nje ya nchi kufanya baadhi ya shooting za nyimbo zake pamoja na kujiweka sawa zaidi kwenye kuchana na huko pia aliweza kufanya baadhi ya nyimbo za raga ambazo amesema nazo zitasikika redioni soon!
Share/Save/Bookmark

No comments:

Post a Comment

 

.