Tuesday, June 1, 2010

UJIO MPYA WA HARD MAD BAADA YA MIAKA MINGI KAPUNI


BAADA YA UKIMYA WA ZAIDI YA MIAKA MITATU HARDMAD AMBAYE NI MSANII MAARUFU KATIKA MUZIKI WA KIZAZI
KIPYA HUSUSAN KATIKA MITINDO YA REGGAE NA RAGGA AMREJEA TENA KWA
KISHINDO. ALBAMU YAKE YA MWISHO AMBAYO ILIWEZA KUFANYA VIZURI ILIKWENDA
KWA JINA LA “NI WEWE”. SAFARI HII MSANII HUYU AMEANZA KWA KUTANGULIZA
SINGO YAKE INAYOITWA “UJIO MPYA” AMBAYO KWA SASA IMESHAANZA KUPIGWA
KATIKA VITUO MBALIMBALI VYA REDIO NA MUDA SI MREFU ITAWEZA PIA KUONEKANA
KWENYE LUNINGA. SINGO HII NI MOJA YA MAANDALIZI YA ALBAMU YAKE
INAYOUFUATA AMBAYO IMETAYARISHWA NA JAKOB POLL PRODUZA RAIA WA DENMARK
AMBAYE KWA SASA ANAISHI NCHINI TANZANIA. KWA SASA HIVI ALBAMU HIYO IPO
KATIKA HATUA ZA MWISHO ZA UKAMILISHAJI UNAOFANYIKA KATIKA STUDIO C4
COPENHAGEN.

Share/Save/Bookmark

No comments:

Post a Comment

 

.