
Naitwa Juma Chillemba,naishi Johannesburg kwa muda mrefu kiasi,nimekuwa siridhishwi na jinsi music videos za kibongo pamoja na movies,talk shows,realty shows,comedy n.k zinavyokuwa hazirushwi hewani kwa wingi katika chnnls za dstv na mnet km vile chanl 0,trace,africa magic na nyinginezo ukilinganisha na kazi za mataifa mengine ya kiafrica wakati bongo kuna wasanii wengi na wenye vipaji vya ukweli pia hata video zetu siku hizi zina ubora wa kutosha.
Kwa uchungu wa kweli nikaamua kwenda makao makuu ya jamaa wa dstv kujua kulikoni,kwa mshangao nikaambiwa na wahusika kuwa wanataka sana kazi mbali mbali za wabongo isipokuwa hawazipati kirahisi km wanavyozipata zingine.wakataja kazi ya mwanadada Shaa kuwa wameipenda sana na wangefurahi sana km wangepata kz zake zingine(naomba mfikishie ujume huu)
Baada ya majadiliano ya muda kidogo tukakubaliana kuwa nikusanye kazi za wasanii wa kibongo nizifikishe kwao kwa preview kisha wazirushe hewani lkn siwezi kufanya kazi hii peke yangu ndio maana nimekuandikia uwahabarishe wadau ikibidi uweke ujumbe huu wazi kwenye blog yako wadau waiperuzi kirahisi.
Kazi hii nitaifanya bure kabisa anachotakiwa kufanya msanii mwenye kazi yake ni kuifikisha kinondoni(DSM)nami nitaichukua pale na kuileta studio zao kwa ukaguzi kwa aliye serious awasiliane nami kwa facebook,email(chillembajuma@yahoo.com)au +27736956002.
Narudia kazi hii nitaifanya bure bileshi.

No comments:
Post a Comment