
mwanamziki wa kizazi kipya mwanadafada ray c ambae wakati huu aekwama nchini kenya baada ya kuzinguana na promota wake aliempeleka nchini humo.Ray c aliviambia vyombo vya habari vya kenya kuwa sababu hasa ya promota huyo kutompa mkwanja wake ni kutokana na promota huyo kumtaka kimapenzi na ray c kumchomolea.
sasa promota huyo anaejulikana kwa jina la sadaat muhindi nae ameibuka na kujitetea kwa kuhoji maswali yafuatayo....kama nilimtaka kimapenzi na akanichomolea kwanini nimemleta kenya baada ya mwezi mmoja na nusu tangu nikutane nae nchini tanzania? je kama nilikua namtaka ningewalipia ticket yeye na boy friend wake Lord eyes waje kenya? je hivyo ndivyo angefanya mtu ambae anamtaka mwanamke kimapenzi? jiulize
awali alidaiwa ray c aliingia mkataba na kampuni ya saadat, ambapo alitakiwa kuwa balozi wa kinywaji kinachoitwa Dash alitakiwa kupiga show katika miji kumi, lakini jumamosi hii akiwa mjini nakuru katika ukumbi wa summit club mambo yaliharibika baada ya ray c kugoma kupiga show, kwa madai kuwa promota huyo alitakiwa amlipe nusu ya pesa walizokubaliana kwenye mkataba.
kwa wakati huu promota saadat amecancel ticket za ndege za ray c na lord eyes baada ya mwanadada kupiga nae kazi na kusema kuwa ataendelea kuwepo nchini kenya na kufanya kazi na promoter wengine.

No comments:
Post a Comment